Pages

Pages

Monday, June 7, 2010

Mrs. Maria Ngowi mama mjasiriamali maarufu nchini Tanzania.


Mama Maria Ngowi ni mmoja ya wajasiriamali maarufu sana nchini Tanzania, safari yake ya ujasiriamali ilianzia alipakuwa shule ya msingi katika mkoa wa Kilimanjaro.Historia yake kwa ufupi anasema
“Nilianza kuuza matunda nyumbani kwa dada yangu na kaka zangu. Sikuishia hapo tu nilitengeneza pia vitu ambavyo vilitengenezwa kwa nyama, iliyokaangwa kwa vitunguu vya majani na pilipili kwa watu wazima na ambayo haikuwa na pilipili kwa watoto, hiyo nyama iliyokaangwa ilikuwa inafungashwa na chapati laini, na kisha kutumbukizwa kwenye mafuta ya moto, kitafunwa, hiki kilikuwa kinatembezwa kwenye nyumba za jirani zipatazo 15 kabla ya saa 12.30 asubuhi, kitafunwa hiki kilijulikana kwa jina la sombiro, inassemekana kwamba, sombiro zenye pilipili zilisambazwa jioni saa 11.00 kwa walevi kilabuni.
Kitafunwa hiki kilizoeleka sana na wenyeji wa pale kiasi kwamba siku kikikosekana ilikuwa ni matatizo kwa wale watumiaji, na pia Maria anasema kitafunwa hiki kiliweza kumpatia pesa nyingi kiasi cha kulipa ada ya shuleni,chakula na matumizi mengine ya nyumbani kama sukari mboga na kadhalika. Biashara hii ilikoma pale alipofaulu kuingia seckondari ya Weruweru kwani hapakuwepo na mtu wa kuiendeleza.
Wakati akiwa sekondari aliweza kujiunga na miradi ya shule yaani utunzaji wa ngombe wa maziwa na utunzaji wa kuku wa nyama na mayai. Maria anasema kutokana na hali halisi ya nyumbani kwao haikuwa nzuri kiuchumi ilibidi awe anabaki shuleni wakati shule zimefungwa na kufanya kazi kwenye mradi wa ngombe na wa kuku ili apatiwe mshahara ambao ulimwezesha kumudu misha yake ya shule. Anasema anamshukuru mwalimu aliyekuwa mkuu wa secondary ya Weruweru wakati huo aliyeweza kumpatia ajira hiyo ambayo alikuwa anamlipa kima cha mishahara ya serikali Tshs. 380/= za mwaka 1977 zilikuwa zinamtosheleza sana kwa mahitaji yote ya shule.
Ni wakati huo ambao Maria anasema aliweza kufungua akaunti yake katika benki ya nyumba na akatunza fedha hizo zikamsaidia mpaka alipokuwa anajiunga na Chuo cha ufundi Dar es salaam Tech. College. Akiwa chuoni hakufanya biashara yeyote kwani walikuwa wanalipwa posho na serekali na kila walipokwenda viwandani kufanya mazoezi (field) alikuwa anapata posho mbili ile ya serikali nay a pale kiwandani.
Alipomaliza chuo alijiunga na jeshi kwa mujibu wa sheria ya Tanzania wakati ule na alianza biashara nyingine ya vitafunwa ambayo ilikuwa ni kuchemsha mihogo na kuuza. Jeshini huwa wanapewa mapumziko saa 11.00 jioni na alitumia mapumziko haya kukimbia kijijini Lusonga na Magagula huko Songea yeye na rafiki yake kununua mihogo na kisha kuichemshia jirani kwa mke wa afande mmoja aliyekuwa jirani na hanga letu. Mihogo hiyo ilikuwa inamenywa jioni na kisha kuchemshwa asubuhi saa kumi ya usiku na kuaza kuuzwa saa 11.00 asubuhi kwa wenzetu na baadaye hata maafande waliinunua bila kujua chanzo cha biashara hiyo.
Maria anaishukuru sana serekali kuwapitisha kwenye mkondo wa jeshi wakati huo kwani aliimarika zaidi na kutotishika na hali yeyote hata ingekuwa ngumu kiasi gani.
Mbali na kuuza mihogo alitumia ustadi wake wa kusuka nywele na kuanza kusuka matroni wa jeshi mke wa mkuu wa kikosi na maafande wengine wanawake waliokuwa na vyeo, hii ilimwondolea kula kwa mstari wa kugombania na kuanza kula chakula kule alikokuwa anasuka nywele. Kipato chake kilikuwa kinaendelea kuwa kizuri kiasi ambacho alipotoka jeshini na kuanza kazi alimudu maisha ya nauli na chakula kwa miezi miwili ya kwanza akisubiri jina lake liingie kwenye pay roll ya serikali.
Mama huyu anatuasa vijana tuwe na utayari wa kukabiliana na maisha tusiwe tegemezi.“Kuwa mjasiriamali kunaitaji kuwa mbunifu, mwenye hekima, mtu aliyeteyari kupambana na aina ya changamoto zozote ili kupenya katika ulimwengu huu wa leo.
Vijana wadogo nawasihi kuutumia muda wenu vizuri sana katika mambo muhimu yakujenga maisha yenu na sio kutumia muda wenu mwingi kubonyezabonyeza simu yaani vimeseji vyote vya Extream badala ya kufikiria vitu vitakavyowasaidia hapo baadaye, hii inasababisha kutoupa ubongo wako kuwe na mapana yakufikiria mambo muhimu kwa upana zaidi.”
. Kila muda unaoupoteza ni lazima utakuja kuujutia au atajisababishia omba omba na kuilalamikia serikali ambayo haijakunyima chochote ila umejinyima mwenyewe.
Kila binadamu kapewa masaa 24 tu kwa siku angalia sana masaa yako unayatumiaje?
Hivi leo mama Maria Ngowi anaendelea na harakati zake za ujasiriamali na kuwafundisha vijana mashuleni,na vyuoni akiwafundisha vijana na kuwaimiza kuwa wajasiriamali katika maisha yao. “Vijana msitegemee sana kuajiriwa, inawezekana kujiajiri wenyewe au hata kama mkiajiriwa muweze kutoa huduma nzuri inayoridhisha.
Mwisho mama huyu anashauri vijana kuulinda utu wao ni muhimu sana, bila nidhamu, utu wema na kumcha Mungu, mtapata hasara nyingi na hata kufikia kupoteza maisha haraka kabla hujafanya kile Mungu alichokutuma duniani.
Kila binadamu aliyekuja hapa duniani ana kazi au (assignment) aliyopewa na Mungu, ni lazima uitafiti uijue na kisha ufanye ipasavyo, la sivyo utafanya kazi za wenzio, utachokea kisichokusaidia na siku yako ya mwisho utakuwa huna kazi ya kuonyesha.
Maisha safi ni silaha kubwa ya kujijengea ujasiri, heshima na ufahamu mzuri. Kila kijana ajitahidi awe na mshauri mzuri mwenye maadili ili akusaidie usije ukajuta baadaye. Wengi wanajuta kwa yale waliyofanya ujanani na sasa wanavuna majuto . usingoje upate majuto la hasha tengeneza maisha yako vizuri ili ule matunda mazuri mbeleni. Kumbuka kila mbegu mbaya unayoipanda utaivuna punde, basi jitahidini kupanda mbegu nzuri.
Mungu awabariki kwa kuzingatia wosia huu.”
Baada ya kumsikiliza mama huyu mimi mwenyewe niliamua niyazingatie haya aliyosema, ameniahidi kipindi kijacho atanieleza ni namna gani, au siri kuu saba za mtu kuishi maisha yenye mafanikio.

5 comments:

  1. Nimeona mwanangu si mchezo, yani we ni mkali!Mi mbona nakukubali si mchezo,kazi na siku njema- Sisy May

    ReplyDelete
  2. Mungu ni mwema,ni safari ngumu sana kimaisha ukimpa mtu wa karne ya juzi juzi hataiweza hata robo,god bless her heart.....

    ReplyDelete
  3. @ Anonymous thanx my dear n Sisy and @ Sis Jiliet 4 sure God z always blassing her...

    ReplyDelete
  4. Kazi nzuri kaka nimeipenda!Mungu akubariki

    ReplyDelete